Tovuti, gazeti na maonyesho ya televisheni ya Dunia wa Kesho , vinakupa majibu ya wazi ya Biblia kwa maswali yaliyo ya muhimu sana: Kwa nini ulizaliwa? Ni kitu gani kitatokea baada ya kifo? Siku za mbeleni zimehifadhi nini? Dunia ya Kesho sio tu inatoa utambuzi sababu za utokeaji wa vichwa vya habari vya hivi hivi sasa, bali tunaeleza, kulingana na unabii wa Bibilia, ni nini kitakacho fanyika siku za usoni.
Kipindi cha televisheni cha Dunia ya Kesho kinacho wekwa hewani katika lugha –Kingereza kimekuwa hewani kwa kila wiki kutoka Januari 1999, kikigawana na mamilioni ya watazamaji majibu ya Biblia kwa maswali muhimu ya maisha: Maisha yako ya usoni yapi na na siku za usoni za dunia zikoje? Ni nini unaweza kufanya ili kupata furaha na mafanikio kwenye maisha haya, na kwa muda mrefu?
Kwa kufanya unabii wa Bibilia uwe raisi kueleweka , Dunia ya Kesho hutoa ukweli kuhusu ni nini kinacho sababisha matukio ya dunia, na kueleza ni nini kitakacho fanyika katika siku zako za usoni. Kama unakumbukumbu ya maonyesho ya televisheni ya zamaniya Dunia ya kesho ya Bw. Herbert W. Armstrong , utambua mafunzo yale yale kwenye vipindi vyetu. Mtayarishi Mkuu Roderick C. Meredith alimsaidia na Bw. Armstrong na baadhi ya vipindi vyake vya redio yake na vipindi mwanzoni vya vya televisheni ukirudi kwenye miaka ya 1950. Mtangazaji wetu mmoja wa Dunia ya Kesho, Bw. Richard F. Ames, alikuwa mtangazaji katika kipindi cha televisheni cha Dunia ya Kesho kwa muda wa miaka kadhaa baada ya kifo cha Bw. Armstrong
Kipindi cha televisheni cha Dunia ya kesho kinatangazia ulimwengu habari nzuri za kuja kwa Ufalme wa Yesu Kristo ( Mathayo 24 :14) na kupiga kwa nguvu “tarumbeta ya onyo” la Siku ya hukumu ya Mungu, ikiita watu kutubu na kubadilika kiroho ( Mathayo 24:21;Isaiya 58:1;Hezekia 33). Tangazo la televisheni pia linatoa vifaa muhimu kuishi kwa mafanikio katika dunia yetu hii ya kutatanisha na kuteta mfadhaiko wa mara kwa mara. Njia za Mungu huleta amani na kuridhika kwa wale wanaoifuata na tuna tumaini kuwa kipindi cha Dunia ya Kesho kitakuwezesha kuwa na “maisha yaliyojaa” (Yohana 10:10) ambayo Mungu anawakutakia.
Kama unaelewa kabisa Kingereza au unaweza kupata mtu wa , kukutafsiria, tunatumaini utafuraia habari zilizomo katika tovuti yetu ya www.tomorrowsworld.org iliyo katika lugha ya Kingereza,.
Hapo , utapata mada za vipindi vya televisheni vyenye muhimu sana katika maisha yako. Baadhi ya vipindi vyetu vinavyopendwa ni:
Kristo Atarudi Lini?
Je,Wafu Wataishi Tena?
Kutatua Rabsha Ya Ukristo
Miaka Hamsini Ya Umoja wa Ulaya
Mbinu Saba Za Udanganyifu Wa Kishetani
Tunaonyesha kipindi kipya cha televisheni kila wiki. Pia tuna chapisha vijitabu vingi ili vikusaidie kuelewa ukweli wa Bibilia yako. Baadhi ya vitabu vyetu vinavyo ombwa mara kwa mara ni:
Ishara Kumi Na Nne Zinazotangaza Kuridi Kwa Kristo
Mashariki Kati katika Unabii
Mambo muhimu Kumi Na Mbili ya Sala Zinazojibiwa
Dunia ya Kesho hutoa Mafunzo ya Bibilia katika lugha ya Kingereza, kwa wanafunzi wanaotaka kwenda ndani zaidi katika kuelewa Neno la Mungu. http://www.twbiblecourse.org/
Gazeti letu la lugha-Kingereza, Dunia ya Kesho, linachapishwa mara sita kwa kila mwaka. Baadhi ya makala ambayo wasomaji wetu wamefurahia ni:
Ukweli Ambao KaribuHakuna Anaeujua!
Mwisho Wa Dunia Na Baadaye
Sababu Saba Kwa Nini Kristo Lazima Arudi!
Ubaguzi Wa Rangi Marekani: Jambo La Kale?
Je, Wakristo Wanapaswa Kutii Siku ya Sabato?
Habari zote zinazotolewa na Dunia ya Kesho zinapatikana bure, bila malipo. Tunafuata kanuni ya Biblia, “Mmepewa bure, toeni bure” (Mathayo 10:8). Tunaweza kufanya hivi kwa sababu ya fungu la kumi na sadaka zinazotolewa na wale walio chagua kutusaidia kama wafanyakazi-wasidizi kwa kutangaza Injili ya kweli ya Yesu Kristo kwa mataifa yote.
Tuna sikitika kuwa kwa sasa tuna wawakilishi wachache, kama wapo, ambaowana ongea lugha yako. Wawakilishi wetu wengi wanaongea Kingereza. Baadhi wanaongea Kifaransa au Kihispania.
Kama unaongea Kifaranza, au unaweza kupata mtu wa kukusaidia kutafsiri , tafadhali katazame tovuti yetu ya lugha ya Kifaransa www.mondedemain.org.
Wanao ongea-Kihispania wanaweza kupendelea tovuti yetu www.elmundodemanana.org.
Tunatumai katika siku za mbeleni, kutafsiri baadhi ya habari zetu katika lugha yako. Kutusaidia tujuwe kiwango cha shauku, tafadhali tujulishe ni habari zetu zipi ungependa kusoma katika lugha yako asili. Kwa sasa, tunatumaini utafurahia habari zetu za Kingereza, Kifaransa na Kihispania.
Ikiwa unataka kuwasiliana katika Kiingereza na Mwakilishi wa Dunia ya Kesho, tafadhali tuma barua-pepe kwa [email protected], au tupigie simu namba (704) 844-1970, au tuandikie kwenye anwani:
Dunia ya Kesho
P. O. Box 3810
Charlotte, NC 28227-8010
Ikiwa unataka kuwasiliana katika Kifaransa na Mwakilishi wa Le Monde de Demain, tafadhali tuma barua-pepe kwa [email protected], au tupigie simu namba (704) 844-1960 x220, au tuandikie kwenye anwani:
Le Monde de Demain
P. O. Box 3810
Charlotte, NC 28227-8010
Ikiwa unataka kuwasiliana katika Kihispania na mwakilishi wa El Mundo de Mañana, tafadhali tuma barua-pepe kwa [email protected], au tupigie simu namba (704) 844-1960 x217, au tuandikie kwenye anwani:
El Mundo de Mañana
P. O. Box 3810
Charlotte, NC 28227-8010